Kibabii University

Call for Abstracts/Papers for a Book to Honor Prof. Ken Walibora

WITO WA IKISIRI/MAKALA YA KITABU KWA HESHIMA YA PROF.KEN WALIBORA

Kutokana  na mchango  mkubwa  aliotoa Profesa   Ken Walibora   katika taaluma  ya Kiswahili   na fasihi kwa ujumla,   Chuo  Kikuu   cha Kibabii   na  Chuo  Kikuu cha  Kisii   vimepanga   kuchapisha    kitabu   cha kumuenzi. Kitabu  hicho kitakuwa   na anwani:  Safari ya Kiswahili ya Ken Walibora.

lkisiri/Makala   yanakaribishwa   katika mojawapo ya maeneo yaliyoshughulikiwa   na Profesa   Walibora, ambayo  ni:

  • Riwaya ya Kiswahili
  • Hadithi Fupi ya Kiswahili
  • Ushairi wa Kiswahili
  • Otobayografia/Bayografia
  • Fasihi ya Kiafrika
  • Lugha ya Kiswahili kwa ujumla
  • Kazi zilizoandikwa  kuhusu  Ken Walibora

MAMBO YA KUZINGATIA  KATIKA  KUANDIKA  MAKALA

landikwe  kwa lugha ya Kiswahili  au Kiingereza. lwe  na maneno  kati ya 3500 – 6000.

lpigwe  chapa katika  programu  ya word,  mtindo  wa Times  New Roman fonti ya 12

Mistari itengane  kwa kipimo  cha nafasi  ya 1.5. Makala iwe na ikisiri.

Makala ihaririwe  vizuri.

Urejeleaji ufanywe kwa kutumia  mtindo  wa APA Toleo  la 8.

Ukurasa wa kwanza  uoneshe  anwani  ya makala, jina la mwandishi   na anwani  yake ya barua  pepe.

TAREHE MUHIMU

08.05.2024    Kutolewa kwa wito wa ikisiri/makala

10.06.2024    Makataa ya kupokea  ikisiri

30.06.2024   Kukubalika/kutokubaika    kwa ikisiri

30.09.2024    Makataa ya kupokea makala

30.01.2025    Kukamilisha  uhariri  wa makala

30.03.2025   Uchapishaji kukamilika

Aprlll 2025  Uzinduzi wa kitabu

Date

May 08 2024 - Jun 10 2024
Ongoing...

Time

8:00 am - 11:00 pm
Category