Kibabii University

Profesa Ken Walibora Alikuwa Mtu Spesheli Asema Profesa Isaac Ipara Odeo

Kikosi cha #Dawati_La_Lugha @West Tv Kenya kikiongozwa na @Dalmus Sakali kilizungumza na Profesa Ipara Odeo, makamu chansela wa chuo kikuu cha Kibabii, mkwasi na mtumiaji mkubwa wa lugha ya Kiswahili.

Katika mazungumzo hayo yaliyomuangazia marehemu Profesa Ken Walibora -mwandishi, mwanahabari na mhadhiri tajika nchini Kenya, Prof Ipara anamtaja bingwa huyo kama mtu wa aina yake, akimlinganisha na mwandishi tajika Shabaan Robert

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp