Call for Abstracts/Papers for a Book to Honor Prof. Ken Walibora
WITO WA IKISIRI/MAKALA YA KITABU KWA HESHIMA YA PROF.KEN WALIBORA
Kutokana na mchango mkubwa aliotoa Profesa Ken Walibora katika taaluma ya Kiswahili na fasihi kwa ujumla, Chuo Kikuu cha Kibabii na Chuo Kikuu cha Kisii vimepanga kuchapisha kitabu cha kumuenzi. Kitabu hicho kitakuwa na anwani: Safari ya Kiswahili ya Ken Walibora.
lkisiri/Makala yanakaribishwa katika mojawapo ya maeneo yaliyoshughulikiwa na Profesa Walibora, ambayo ni:
- Riwaya ya Kiswahili
- Hadithi Fupi ya Kiswahili
- Ushairi wa Kiswahili
- Otobayografia/Bayografia
- Fasihi ya Kiafrika
- Lugha ya Kiswahili kwa ujumla
- Kazi zilizoandikwa kuhusu Ken Walibora
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUANDIKA MAKALA
landikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza. lwe na maneno kati ya 3500 – 6000.
lpigwe chapa katika programu ya word, mtindo wa Times New Roman fonti ya 12
Mistari itengane kwa kipimo cha nafasi ya 1.5. Makala iwe na ikisiri.
Makala ihaririwe vizuri.
Urejeleaji ufanywe kwa kutumia mtindo wa APA Toleo la 8.
Ukurasa wa kwanza uoneshe anwani ya makala, jina la mwandishi na anwani yake ya barua pepe.
TAREHE MUHIMU
08.05.2024 Kutolewa kwa wito wa ikisiri/makala
10.06.2024 Makataa ya kupokea ikisiri
30.06.2024 Kukubalika/kutokubaika kwa ikisiri
30.09.2024 Makataa ya kupokea makala
30.01.2025 Kukamilisha uhariri wa makala
30.03.2025 Uchapishaji kukamilika
Aprlll 2025 Uzinduzi wa kitabu