Chama cha Kiswahili Kibabii (CHAKIKI) kilizinduliwa mnamo 27/11/2015 naye Profesa Ken Waliaula Walibora. Uzinduzi huu ulijiri mara tu baada ya Kibabii kupewa hadhi ya kuhudumu kama chuo kikuu Jumamosi 14/11/2015 baada ya kuhudumu kama tawi la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro kwa takriba miaka mitatu.

CHAKIKI kilianza kazi zake chini ya Bw. Anthony Oloo Owino akiwa mlezi wake.Bw Oloo alishikilia nafasi hii na hatimaye kumkabithi Dkt Simiyu ambaye hadi sasa, 2018,bado ndiye Mlezi wa chama hiki cha CHAKIKI. Hata hivyo, katika utendakazi wake, CHAKIKI kilionekana fifi kwani shughuli zake nyingi hazikuwa zikiendeshwa. Chini ya Mlezi Owino Oloo Anthony, kulikuwepo viongozi wafuatao;Victor(Mwenyekiti),Janet Bosibori (makamu mwenyekiti) Bonface Ambaka (Mhariri) na Imani Enock (mhazini).

Kipindi hicho cha mwanzo kiliwavutia takriban wanachuo ishirini ambao walijiandikisha kama wanachama kamili. CHAKIKI kilikaa hafifu hata tarehe 9/2/2018 kikao cha mwanzo kilipoandaliwa idarani mwa Kiswahili chini ya uelekezi wa Daktari Simiyu. Kikao hicho kiliwaleta pamoja wawakilishi wa wanafunzi wa Kiswahili chuoni na wapenzi wengine wa Kiswahili. Kikao chenyewe kilihudhuriwa na wanachuo kumi ambao ni Bonface Ambaka, Stephen Barng’etuny,Willington Wakukha, Billy Mandela Jomo , Sifuna W. Peter, Joel Muricho, Wangulo Philemon, Imbeka L. Victor,Douglas Ouma Wango na Nandwa Zablon.

Mkutanoni humo, kaimu viongozi walichaguliwa kusimamamia nyadhifa mbalimbali.Nyadhifa hizi zilikuwa;Mwenyekiti-Bonface Ambaka, Naibu mwenyekiti -Nandwa Zablon, Katibu Mkuu -Stephen Barng’etuny,Naibu Katibu Mkuu -Mercy Erima, Mhazini -Janet Bosibori, Mhariri Mkuu -Willington Wakukha na Naibu mhariri -Wafula Peter.Toka hapo, CHAKIKI kilifufuliwa kwa wanachuo kuhamasishwa kujiunga na chama hiki ambapo baadhi ya wanachuo walijitokeza na kujiandikisha japo ilikuwa idadi ndogo.

Baadaye kama mwamko mpya, CHAKIKI kiliwakilisha Chuo Kikuu cha Kibabii katika kongamano la kitaifa la Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki kanda ya Kenya(CHAWAKAMA-KENYA)lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kenyatta tarehe 17/2/2018 ambapo wanachama kumi na watatu walishiriki.Kaimu Katibu Mkuu chini ya idara ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika, aliandika barua kwa afisi kuu ya CHAWAKAMA-KENYA ya kuomba uana chamani humo.Kufuatia mwamko huu, tarehe 10/11/2018 CHAKIKI wakati huo kama mwanachama katika CHAWAKAMA-KENYA, kilihudhuria kongamano lake katika Chuo Kikuu cha Egerton Bewa Kuu-Njoro ambapo wanachama 47 walishiriki.

Kwa sasa CHAKIKI kimeanza kazi zake kwa kasi na hivi karibu kitakuwa kinatoa majarida na fulana kwa ajili ya wanachama wake na jamii ya Kibabii kwa jumla. Misururu ya mikutano imekuwa ikiandaliwa na chama hiki kama njia moja ya kuzidi kukuza chama hiki. Usajili pia wa wanachama wapya unazidi kwani idadi ya upeo wa memba bado haijafikiwa.


[pt_view id=”6f744922rx”]