Kikosi cha #Dawati_La_Lugha @West Tv Kenya kikiongozwa na @Dalmus Sakali kilizungumza na Profesa Ipara Odeo, makamu chansela wa chuo kikuu cha Kibabii, mkwasi na mtumiaji mkubwa wa lugha ya Kiswahili.
Katika mazungumzo hayo yaliyomuangazia marehemu Profesa Ken Walibora -mwandishi, mwanahabari na mhadhiri tajika nchini Kenya, Prof Ipara anamtaja bingwa huyo kama mtu wa aina yake, akimlinganisha na mwandishi tajika Shabaan Robert