Na Ammar Kassim
Chuo Kikuu cha Kibabii kilianza kampeni yake ya kufuzu kwa michuano ya vyuo vikuu nchini (KUSA) kwa kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya chuo cha Kaimosi.
Kibabii ilionekana kudhibiti mchezo katika dakika za mwanzo kwa kuwapiga wenyeji Kaimosi bao la mapema. Bao hilo lilifungwa na difenda Aguastine Shikuku aliyepiga mkwaju wa ikabu uliomzidi nguvu mlinda lango wa timu ya Kaimosi.