Off Bungoma-Chwele Road
sgs@kibu.ac.ke
+254721589365
Dr. Robert Kati
Office Hours: Monday–Friday
8:00 AM – 5:00 PM
sgs@kibu.ac.ke
Dr. Robert Kati
8:00 AM – 5:00 PM
Lengo la makala hii ni kuchunguza mikakati inayotumiwa na viongozi kukabiliana na changamoto zinazokumba uafikiaji wa MME katika tamthilia teule za Kiswahili. Uongozi ni suala muhimu katika jamii na hudhihirika kupitia mikakati kadhaa, mojawapo ni utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME). Utekelezaji wa MME unaendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali. Utafiti huu ni wa kithamano na uliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt (1980) na kuendelezwa na Brizee na Tompkins (2012). Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Data ilikusanywa kupitia mbinu ya unukuzi. Data hii ilipangwa kisha kuchanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia nne ziliteuliwa. Tamthilia hizi ziliteuliwa kwa msingi kuwa zina maudhui ya uongozi na ziliandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2024 ambacho ni kipindi cha utekelezaji wa mpango wa MME. Hizi ni: Shamba la Halaiki (Okello, 2016), Mwinyi na Manyani ya Adili (Mbogo, 2022), Kifunganjia (Okello, 2021) na Kodi (Muhando, 2024). Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya maandishi. Matokeo ya kazi hii ni kuwa, viongozi wanatumia mikakati mbalimbali kukabiliana na changamoto zinazotatiza uafikiaji wa mpango wa MME. Isitoshe, kushiriki na kuhimiza kilimo ni mkakati ambao unachangia uafikiaji wa malengo kadhaa ya MME. Makala ii inapendekeza kuwa viongozi wawashirikishe raia katika utekelezaji wa mikakati inayolenga kuafikia MME ili maendeleo yaafikiwe kwa pamoja. Aidha, viongozi wa nchi mbalimbali waweke mikakati ambayo itainua sekta ya kilimo kuanzia mashinani kwa kuwa kilimo kitasaidia uafikiaji wa malengo kadhaa ya mpango wa MME.