Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya Kupitia Nyimbo Pepe

Student’s Name:
Stephen Muyundo Ndinyo

Supervisors:
1. Prof. Ernest Sangai Mohochi
2. Dr. Joseph Juma Musungu

Doctor of Philosophy in Kiswahili Studies

IKISIRI

Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka yanayotatiza jamii pakubwa huku maendeleo katika vyombo vya habari hususan mtandao yakichangia tatizo hili. Uraibu wa dawa za kulevya ni mwiba katika jamii unaoangaziwa katika nyimbo pepe za kizazi kipya. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa: Kufafanua mtindo ulivyotumika kuwasilisha nyimbo pepe za kizazi kipya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya; kujadili upekee wa uwasilishaji wa nyimbo pepe za kizazi kipya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya; kubaini hatua zinazochukuliwa kudhibiti nyimbo pepe za kizazi kipya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na Kujadili mchango wa nyimbo pepe za kizazi kipya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na Marshall McLuhan’s katika mwaka wa 1964 na ile ya Utendaji iliyoasisiwa naye Wallace Bacon katika mwaka wa 1984. Utafiti huu ulitumia mkabala wa kithamano muundo wa kiutendaji. Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Video za nyimbo pepe za kizazi kipya kuhusu dawa za kulevya zilichanganuliwa katika mtandao wa YouTube. Umma lengwa ulihusisha nyimbo pepe za kizazi kipya na mtandao. Mbinu za usampulishaji wa kimaksudi na kitabaka zilitumika kuchagua nyimbo pepe za kizazi kipya, suala la dawa za kulevya na mtandao wa YouTube. Matokeo ya utafiti huu ni; kwanza, mtindo ulijitokeza kupitia vipengele vya takriri, kuchanganya msimbo, maswali balagha, tashbihi, tashihisi na taswira katika nyimbo pepe za kizazi kipya matandaoni. Pili, upekee wa video za nyimbo pepe za kizazi kipya ulijitokeza katika vigezo vitano vikuu ambavyo ni matumizi ya dawa za kulevya, kucheza dansi, kipengele cha mandhari, kipengele cha jinsia na kile cha umri katika nyimbo pepe za kizazi kipya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Tatu, wimbo mmoja pepe teule wa kizazi kipya uliainishwa katika kategoria ya filamu za kutazamwa na watoto chini ya uongozi wa wazazi wao. Nyimbo zilizosalia nne zikiainishwa katika kategoria ya pili iliyohusisha filamu zinazofaa kutazamwa na jamii nzima. Mwishowe, nyimbo pepe za kizazi kipya zilitumika kwa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na kuangazia athari zake kwa jamii. Lebo za chupa nazo ziliraruliwa, makopo yalionyeshwa bila ya kuonyeshwa kwa pombe. Athari ya uvutaji wa sigara na bangi ilisawiriwa, kushirikishwa kwa vyombo vya habari, kubebwa kwa mabango na kuvaliwa kwa mavazi yenye ujumbe. Ondoa Simiyu.