Off Bungoma-Chwele Road
sgs@kibu.ac.ke
+254721589365
Dr. Robert Kati
Office Hours: Monday–Friday
8:00 AM – 5:00 PM
sgs@kibu.ac.ke
Dr. Robert Kati
8:00 AM – 5:00 PM
Fasihi, kupitia utambuzi na tanzu zake tofauti tofauti, tangu jadi imekuwa na majukumu mahususi ya kutekeleza katika jamii.Vichekesho kama utanzu mojawapo wa Fasihi simulizi, vimetumika pakubwa katika vyombo vya habari kama vile runinga na redioni kufurahisha na kuwachekesha watazamaji na wasikilizaji. Hata hivyo, katika karne 21, futuhi imechukua mkondo tofauti katika uwasilishaji wake. Hii ni kwa sababu ya njia mpya za mawasiliano kwa sababu ya teknolojia ya kisasa ambayo imezua mitandao ya kijamii kama vile Facebook, TikTok, Twitter na YouTube. Mbinu mpya za teknolojia zipo kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote. Licha ya mkurupuko wa mbinu hizi, isisahaulike kwamba tangu jadi futuhi imekuwa muhimu katika jamii mbalimbali. Kwa hivyo, futuhi imekuwa karibu zaidi kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Kwa hivyo, futuhi imetumiwa kukabiliana na masuala ibuka katika jamii nchini Kenya kama vile ndoa, magonjwa kama Korona, siasa, ufisadi, dawa za kulevya, migomo, maandamano, haki za watoto na malezi. Hivyo basi, kulikuwa na haja ya kuchunguza zaidi kuhusu futuhi katika mitandao hii ya kijamii na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, hii ni kwa sababu suala la afya ya akili limeendelea kuwa nyeti nchini. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kudhihirisha sifa bainifu za kisanaa za futuhitandao zinazokabiliana na masuala ya afya ya akili, kupambanua masuala yanayowakumba Wakenya kama yanavyojitokeza ndani ya futuhitandao; na kudadavua dhima ya futuhitandao katika kukabiliana na masuala ya afya ya akili. Mada hii ilichaguliwa kwa sababu tafiti ambazo zilihusu futuhi ziliegemea futuhi katika vitabu vya riwaya na tamthilia na hazikujikita katika suala la afya ya akili. Hivyo basi, utafiti huu ulinuia kujaza pengo hili kwa kutafitia futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, na hasa kwa kuzingatia futuhi zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebook, Twitter na YouTube. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili: Nadharia ya Burudiko iliyoasisiwa na Sigmund Freud (1905) na Nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa na Jacobson na Murry (1960). Utafiti huu ulitumia muundo wa kiethnografia, mkabala wa kithamano. Data kuhusu futuhitandao ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo.Tulitumia Google kama kifaa cha kukusanya data. Umma lengwa ulihusisha futuhi za mtandaoni. Utafiti huu ulitumia mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi na kinasibu. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa, kuna uhusiano baina ya futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa, matokeo yake yamedhihirisha kuna uhusiano baina ya futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya na kuonesha kuwa, futuhitandao ni tiba mbadala au ni therapia katika kukabiliana na masuala ya afya ya akili.