Off Bungoma-Chwele Road
sgs@kibu.ac.ke
+254721589365
Dr. Robert Kati
Office Hours: Monday–Friday
8:00 AM – 5:00 PM
sgs@kibu.ac.ke
Dr. Robert Kati
8:00 AM – 5:00 PM
Fasihi kupitia utambuzi na tanzu zake tofauti tofauti, tangu jadi, imekuwa na majukumu mahususi ya kutekeleza katika jamii. Kama utanzu mojawapo wa fasihi simulizi, futuhi imetumika pakubwa katika vyombo vya habari kama vile televisheni na redioni kuwafurahisha na kuwachekesha watazamaji na wasikilizaji. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, futuhi imechukua mkondo tofauti katika uwasilishaji wake. Hii ni kwa sababu ya njia mpya ya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa ambayo imezua mitandao ya kijamii kama vile Facebook, TikTok, Twitter, Instagram na YouTube. Mbinu mpya za kiteknolojia sasa zipo kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote. Licha ya mkurupuko wa mbinu hizi, tusisahau kwamba tangu jadi futuhi imekuwa muhimu katika jamii mbalimbali. Lakini sasa futuhi imekuwa karibu zaidi kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Vile vile, suala la afya ya akili limekuwa nyeti miongoni mwa Wakenya. Hivyo basi, kukawa na haja ya kuchunguza zaidi kuhusu futuhi katika mitandao hii ya kijamii na afya ya akili miongoni mwa Wakenya. Mada hii vile vile ilichaguliwa kwa sababu tafiti ambazo zilihusu futuhi, ziliegemea futuhi katika vitabu vya riwaya na tamthilia na hazikujikita katika suala la afya ya akili. Hivyo basi, makala haya yalinuia kujaza pengo hili kwa kutafitia futuhitandao na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, na hasa kwa kuzingatia futuhi zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebook, Twitter na YouTube. Makala haya yalitumia nadharia ya Burudiko ya Sigmund Freud. Utafiti huu ulitumia muundo wa kiethnografia, mkabala wa kithamano. Data kuhusu futuhitandao ilikusanywa kwa mbinu ya Uchanganuzi wa Yaliyomo. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimakusudi na kinasibu. Umuhimu wa makala haya ni kuwa, matokeo yake yatasaidia katika ufundishaji wa futuhi. Inapendekezwa kuwa tafiti zaidi zifanywe kuhusu suala la afya ya akili kwa kurejelea vipera vingine vya fasihi simulizi.