Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Athari za Aina za Uchawi na Taashira zake katika Utekelezaji wa Malengo ya Elimu Nchini Kenya: Mfano wa hadithi fupi teule za kiswahili

2025

Authors

Shikanda Paul Andrew Kaggwa
Wanjala Fred Simiyu
Simiyu Benson Sululu

Abstract

Makala haya yanadadavua jinsi ambavyo aina na taashira za uchawi zinavyoathiri utekelezaji wa malengo ya elimu nchini Kenya, yakirejelea hadithi fupi teule za kufundisha fasihi ya Kiswahili. Tafiti nyingi za fasihi ya Kiswahili zimeegemea tanzu za riwaya, tamthilia na ushairi kuhusu uchawi. Hata hivyo, tafiti hizo hazijarejelea aina na taashira za kiuchawi katika utekelezaji wa malengo ya elimu haswa kwa mujibu wa hadithi fupiza kufundishia fasihi ya kiswahili. Uchunguzi huu umejikita katika mihimili ya nadharia ya uchawi iliyoasisiwa na Pritchard Edward (1939). Nadaria hii inachukulia kuwa uchawi ni tukio la kijamii na kuelewa utamaduni na muktadha halisi wa jamii husika. Utafiti huu ni wa mkabala wa kithamano, muundo wa kimfano. Idadi lengwa ya utafiti ni hadithi fupi teule 6 kutoka kwa diwani 5, na malengo 2 kati ya 8 ya elimu nchini Kenya. Mbinu ya ukusanyaji data ilikuwa uchanganuzi wa yaliyomo na kuchanganuliwa kwa kutumia uchanganuzi wa nyaraka na kuwasilishwa kwa maelezo ya kina. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba aina za uchawi na taashira zake zinawezatumika kuendeleza maadili na utamaduni miongoni mwa wanafunzi na jamii kwa jumla. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu, wanafunzi, waandishi wa hadithi fupi teule na jamii husika kwa jumla.Ipo haja ya Wizara elimu na washika dau kuandaa warsha na seminaa za kuhamasisha jamii kuhusu kuhifadhi na kuthamini tamaduni za jamii kupitia tanzu za fasihi hasa hadithi fupi