Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni

2025

Authors

Stephen Muyundo Ndinyo
Ernest Sangai Mohochi
Joseph Juma Musungu

Abstract

Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964). Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika. Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoniUmma lengwa ulihusisha nyimbo za kizazi kipya na mtandao. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za kulevya na mtandao wa You Tube. Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika utabakisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati iliyosawiriwaJumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa. Kazi hii ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo. Matokeo ya kazi hii ni kwamba nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya mihadarati. Makala haya yanapendekeza mitandao mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya mihadarati. Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya. Hatimaye, madhara ya mihadarati pia zitafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga.