Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Uimarishaji wa Lugha za Kiasili Kupitia Vyombo vya Habari: Mfano wa Kinandi katika Runinga ya Kass

2025

Authors

Melly Kipchirchir Joachim
Eric Walela Wamalwa
Ernest Sangai Mohochi

Abstract

Lugha za kiasili ni muhimu sana katika kufanikisha mawasiliano kwa kuwa hutumiwa na watu wengi. Hata hivyo lugha hizi zinapitia changamoto kwa kuwa idadi ya wazungumzaji inazidi kupunguka. Hii ni kwa sababu lugha hizi zinapuuzwa huku lugha za Kiswahili na Kingereza zikitukuzwa. Hali hii inawafanya watu wengi kutumia Kiswahili katika mawasiliano ya mara kwa mara. Kutokana na umuhimu wa lugha za kiasili, ipo haja ya kuziimarisha. Makala hii inafafanua jinsi vipindi vya kilimo katika runinga ya Kass vinachangia katika uimarishaji wa lugha ya Kinandi. Uchunguzi uliozaa makala hii ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Mawasiliano ya Sperka (1966). Washiriki 264 waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika uchunguzi. Mbinu za hojaji, utazamaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Data zilikusanywa kwa kutumia mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kitakwimu na kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha zikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Kutokana na uchunguzi huu, tumetambua kuwa lugha ya Kinandi inaweza kuimarishwa kupitia njia zifuatazo: Kuhimiza matumizi ya Kinandi katika mawasiliano ya mara kwa mara, kuwafundisha watoto kama lugha ya kwanza, kufundisha shuleni kama mojawapo ya masomo, kuhimiza matumizi katika vyombo vya habari na kuhifadhi kwenye maandishi.