Off Bungoma-Chwele Road
sgs@kibu.ac.ke
+254721589365
Dr. Robert Kati
Office Hours: Monday–Friday
8:00 AM – 5:00 PM
sgs@kibu.ac.ke
Dr. Robert Kati
8:00 AM – 5:00 PM
Wakulima wengi nchini Kenya hupatikana katika maeneo ya mashambani ambako mawasiliano mengi huwa katika lugha za kiasili. Vyombo vya habari ni miongoni mwa asasi ambazo zimechangia pakubwa katika kukuza matumizi ya lugha za kiasili na kuwahamasisha wananchi kuhusu kilimo. Kwa sababu hiyo, juhudi nyingi zimeelekezwa katika kuwafikia wakulima ambao ni wahusika wakuu katika sekta ya kilimo ili kuwapa elimu ya kujiendeleza. Lugha ya Kinandi ni mojawapo ya lugha za kiasili ambayo hutumiwa katika runinga ya Kass. Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi lugha ya Kinandi hutumika kuinua viwango vya kilimo miongoni mwa wanajamii kupitia vipindi vya runinga ya Kass. Utafiti huu ulifanyika katika kaunti ya Nandi. Uliongozwa na Nadharia ya Uanzilishi wa Ajenda ya McCombs na Shaw (1993). Watazamaji waliteuliwa kinasibu ili kuhusishwa katika utafiti. Watazamaji 264 walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Mbinu za hojaji, uchunzaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Vifaa vilivyotumika kukusanya data ni: mwongozo wa utazamaji, hojaji na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti kisha ikawasilishwa kwa kutumia asilimia na majedwali. Matokeo ya utafiti yalithibitisha kuwa lugha ya kinandi inayotumika kuwasilisha vipindi vya kilimo iliwasaidia sana wakulima kuimarisha mapato katika kilimo. Utafiti huu unatarajiwa kuwa wa manufaa kwa wanajamii kwa kuwa ulitoa mwanga kuhusu umuhimu wa matumizi ya lugha za kiasili katika kuinua viwango vya kilimo.