Off Bungoma-Chwele Road
sgs@kibu.ac.ke
+254721589365
Dr. Robert Kati
Office Hours: Monday–Friday
8:00 AM – 5:00 PM
sgs@kibu.ac.ke
Dr. Robert Kati
8:00 AM – 5:00 PM
Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni miongoni mwa masuala yanayosawiriwa katika nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Katika kufanya hivyo, nyimbo hizo hutumia vipengele mbalimbali vya kisanii. Mojawapo kati ya vipengele hivyo ni mandhari, huku usukaji mzuri wa mandhari ukichangia fanaka katika uwasilishaji wa ujumbe wa nyimbo hizo. Makala haya yalichunguza mandhari katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Makala yaliongozwa na Nadharia ya Utendaji katika Fasihi Simulizi iliyoasisiwa na Wallace Bacon katika mwaka wa 1957. Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika katika makala haya. Uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data kutoka kwa video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu dawa za kulevya katika mtandao wa YouTube ambao uliteuliwa kimaksudi. Aidha, nyimbo ziliteuliwa kimaksudi. Kisha, nyimbo hizo zilitabakishwa kidhima na kwa kurejelea aina tofauti za dawa za kulevya zinazosawiriwa. Jumla ya nyimbo 5 zilitumika. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi na mijadala, mifano na dondoo kutoka kwenye uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionyesha kwamba aina mbalimbali ya mandhari yalibainika katika video za nyimbo za kizazi kipya kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya mtandaoni. Mandhari ya klabu, nyumbani, barabarani, mjini, mtaani na yale ya wakati yalitumika katika vita dhidi ya uraibu wa dawa za kulevya katika jamii. Aina hizi za mandhari zilotoa mchango katika kuwasilisha ujumbe kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya. Utafiti unapendekeza kwamba kuna haja ya kuchunguza mandhari kuhusiana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kurejelea aina nyinginezo za nyimbo mbali na zile za kizazi kipya. Pili, ni vyema mandhari yatafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga kwa kurejelea suala la dawa za kulevya