Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Sifa Bainifu za Futuhitandao katika Kukabiliana na Afya ya Akili Miongoni mwa Wakenya

2025

Authors

Magambo Emilly Angushi
Simiyu Fred Wanjala
Orina Felix Ayioka

Abstract

Futuhi imetumika pakubwa katika vyombo vya habari kama vile televisheni na redioni kufurahisha na kuwachekesha watazamaji na wasikilizaji. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, futuhi imechukua mkondo tofauti katika uwasilishaji wake. Hii ni kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Kulikuwa na haja ya kuchunguza zaidi kuhusu futuhi katika mitandao ya kijamii na afya ya akili miongoni mwa Wakenya, hii ni kwa sababu suala la afya ya akili limeendelea kuwa suala nyeti nchini Kenya. Makala haya yalilenga hasa kudhihirisha sifa bainifu za kisanaa kwenye futuhitandao zinazokabiliana na masuala ya afya ya akili. Mitandao ya kijamii iliyohusishwa ni Facebook, Twitter na YouTube. Utafiti uliongozwa na nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Jacobson na Murry. Usampulishaji wa kimakusudi na kinasibu zilitumiwa ili kupata data. Data kuhusu futuhitandao ilikusanywa kwa mbinu ya Uchanganuzi wa Yaliyomo. Data iliwasilishwa kwa njia ya maelezo ya kiufafanuzi. Sifa zilizobainika za futuhitandao ni pamoja na: Futuhitandao huashiria unyume (antonimia), huzingatia itikadi za kijamii, huwasilisha ujumbe mzito kwa njia ya moja kwa moja, husheheni takriri, kejeli, huwasilishwa kwa njia ya moja kwa moja, hujaa chuku, kinaya na mwendo wake huwa wa kasi. Makala haya yalipendekeza kwamba haja ipo ya kuchunguza aina nyinginezo za maigizo tofauti na futuhitandao katika kukabiliana na afya ya akili miongoni mwa Wakenya. Pili, ni vyema afya ya akili miongoni mwa Wakenya katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile nyimbo, filamu na vipindi vya runinga kwa kurejelea suala la dawa za kulevya. Mwishowe, ni muhimu kukabiliana kwa suala la afya ya akili pia urejelewe kwa aina nyinginezo za maigizo mbali na futuhitandao