Off Bungoma-Chwele Road

sgs@kibu.ac.ke

+254721589365

Dr. Robert Kati

Office Hours: Monday–Friday

8:00 AM – 5:00 PM

Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili

2025

Authors

Samuel Sinzore Ogonda
Isaac Odeo Ipara
Amukowa Deborah

Abstract

Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt mwaka wa 1980. Utafiti huu ni wa kithamano na ulitumia muundo wa kiuchanganuzi. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kukusanya data.  Data ilipangwa kisha kuchanganuliwa kupitia Mbinu ya uhakiki wa yaliyomo. Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia nne ziliteuliwa. Tamthilia hizi ziliteuliwa kwa msingi kuwa zina maudhui ya uongozi na ziliandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2024. Hizi ni: Shamba la HalaikiMwinyi na Manyani ya AdiliKifunganjia na Kodi. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya kazi hii ni kuwa kuna aina mbili kuu za uongozi zinazojitokeza katika tamthilia teule za Kiswahili: uongozi wa kidemokrasia na wa kidikteta. Demokrasia iliendeleza uafikiaji wa MME kinyume na udikteta uliodumaza uafikiaji wa MME. Makala haya yanapendekeza kuwa wananchi katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu wachangie uongozi bora katika jamii zao ili kufanikisha uafikiaji wa MME. Aidha, watafiti wa baadaye walinganishe na kulinganua aina mbalimbali za uongozi katika kazi mbalimbali za fasihi kando na uongozi wa kidemokrasia na kidiktea ulioshughuliwa katika makala haya.